WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mh Selemani Jafo, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ndg Aron Kagurumjuli pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dar es salam, Ndg Sipora Liana kwa utendaji wao wa kazi uliotukuka.
Jafo ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi na uwekaji sahihi mikataba ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika mamlaka za serikali za mitaa.
Amesema viongozi hao ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine wa utumishi wa umma kwa namna ambavyo wanathamini na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
Ameongeza kuwa licha ya Mkurugenzi wa kinondoni kuwa na umri mkubwa, lakini bado amekuwa akichapa kazi kikamilifu kwa kuongoza Manispaa yake na kuhakikisha inapiga hatua katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema asilimia kubwa ya miradi inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ni mawazo na ubunifu wa Mkurugenzi huyo.
Jafo ametoa wito kwa wakurugenzi wengine kuiga mfano wa viongozi hao, huku akiwataka kufanya kazi Kwa bidii na uadilifu kama ambavyo kanuni za utumishi wa umma zinavyotaka.
Katika hafla hiyo uongozi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, waliweka saini katika mradi was Ujenzi wa kituo cha mabasi Mbezi Luis huku Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni ukiweka saini katika mradi wa soko la kisasa Magomeni.
Jafo ameahidi kushughulika na wakurugenzi wazembe katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wakurugenzi wote watakaobadilisha matumizi ya fedha za miradi hiyo na kupeleka katika shughuli nyingine.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.