Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM), Dkt. Emmanuel Shindika, amewataka Walimu wa Manispaa ya Kinondoni kuwa sehemu ya kuhakikisha chakula kinachoandaliwa Shuleni kwa ajili ya Wanafunzi kuwa cha asili na chenye virutubisho muhimu.
Dkt. Shindika aliyasema hayo Juni 19, 2024 katika Kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Kiramuu Mbezi Beach, kilichowahusisha Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi, Maafisa Elimu ngazi ya Kata pamoja na Wilaya kwa lengo la kukumbushana majukumu yao ya kila siku katika kukuza ufaulu wa Wanafunzi wao.
Dkt. Shindika alisema, lengo la Serikali kuratibu masuala ya chakula kwa Wanafunzi wanapokuwa shuleni ni jema na linalenga kukuza ufanisi na uelewa mkubwa kwa Wanafunzi wao. "Katika kuhakikisha lengo na maono ya Serikali yanatimia, Walimu tunapaswa kuhakikisha chakula kinachoandaliwa vizuri na chenye lishe bora kwa Watoto."
Aidha, Dkt. Shindika aliwataka Walimu hao kutembea kifua mbele kwa kuwa Taifa la kesho lipo mikononi mwao hivyo wanapaswa kutimiza majukumu yao kwa weledi huku wakiwaandaa Watoto hao vyema kwa ulaji unaojitosheleza.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.