Baraza la madiwani Manispaa ya Kinondoni katika kikao chake leo limepitisha takribani sh biloni 242.1 zikiwa ni fedha kwa ajili ya makadirio ya Mapato na matumizi ya kawaida pamoja na mpango wa bajeti wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019
Akifafanua mpango huo wa matumizi pamoja na bajeti hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamin Sitta amesema kiasi cha takribani bilioni 120.3 ni matumizi ya kawaida, na bilioni 121.8 ni fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo ambapo kiasi cha takribani bilioni 32.7 kinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vyake vya ndani, na bilioni 209.4 ni ruzuku kutoka Serikali kuu kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kutekeleza miradi ya Maendeleo.
Meya Sitta amebainisha kuwa mpango huu wa bajeti umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, Sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, pamoja na hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Joseph Magufuli ya tarehe 20/11/2015.
Nyingine ni malengo ya Maendeleo endelevu ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, Sera ya Taifa ya UKimwi, Sera za kisekta, mipango shirikishi jamii ya fursa na vikwazo ya (O&OD),pamoja na kutekeleza miradi ya kimkakati ili kukuza Mapato ya ndani ya Halmashauri na kutekeleza miradi michache yenye matokeo makubwa kwa haraka.
Naye Mh Songoro Mnyonge diwani kata ya Mwananyamala, ambaye pia ni mwenyekiti kamati ya Mipangomiji na Mazingira akiunga mkono hoja ya kupitishwa kiasi hicho cha fedha amesema Manispaa imejipanga kuibua vyanzo vipya vya mapato ili iweze kukidhi matakwa ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.
Katika hatua nyingine Meya sitta ameainisha vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato, kuboresha miundombinu ya kiafya, shule, barabara, maji, kilimo mjini na vijijini, hifadhi ya Mazingira ukusanyaji wa taka, pamoja na kuboresha Mazingira ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
Imetolewa na
Kitengo chá Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.