Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wameombwa kushawishi na kukaribisha wawekezaji katika kuipa thamani taka.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Manispaa ya Mjini, Zanzibar, Bi. Mwajuma Ally Abadi wakati akitoa taarifa ya shughuli za usafi Baraza la Manispaa Mjini kwa Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni waliofanya ziara Mjini Zanzibar.
Amesema, " Tunakaribisha wawekezaji katika kuipa thamani taka. Taka ni fursa na siyo uchafu, hivyo tunahitaji wawekezaji wenye uwezo na sifa ya kusimamia na kukusanya taka".
Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo Mjini Zanzibar.
Naye Diwani wa Kata ya Wazo, Mheshimiwa Leonard Tungaraza Manyama, akichangia taarifa hiyo, alieleza kuwa kwa Sasa Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Ujerumani, wameanzisha kiwanda cha kuchakata mbolea inayotokana na taka. Kiwanda hicho kipo Mabwepande jijini Dar es Salaam.
Aidha, Bi. Mwajuma amewaeleza Madiwani hao kuwa wapo katika mchakato wa kufikiria kuwasilisha mabadiliko ya viwango vya tozo za taka ili ziendane na wakati wa sasa.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano, Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.