Mashirika na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya kupunguza Kasi ya maambukizi ya VVU Manispaa ya Kinondoni yametakiwa kuhakikisha yanaongeza nguvu katika kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya kupima na kujua afya zao mapema.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi Manispaa hiyo Mh George Manyama alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea taasisi zinazojihusisha na maswala ya kupunguza maambukizi ya VVU. na UKIMWI ambapo taasisi ya JHPIEGO na ICAP zimetembelewa.
Amesema wananchi bado wanahitaji elimu ya kutosha ili waweze kuishi kwa kuzingatia misingi na masharti katika kuzilinda afya zao ambapo amebainisha mashirika mengi kuweka nguvu katika kujua takwimu za Watu waliopata maambukizi na wasiopata maambukizi hali isiyotoa nafasi kwao kuijua afya yake na kujilinda.
Kwa upande wake Mratibu wa kudhibiti ukimwi Manispaa ya Kinondoni ( CHAC), Bi Rhobi Gwesu amesema ipo changamoto kwa baadhi ya makundi ya jamii ambayo hayana uelewa wa kutosha kuhusiana na virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe.
Amelitaja kundi hilo kuwa ni kundi la walemavu,na hivyo Manispaa imejipanga kutoa elimu zaidi ya maswala hayo ya vvu na Ukimwi ili waweze kujilinda.
Kamati ya kudhibiti maambukizi ya VVU (Ukimwi) Manispaa ya Kinondoni inashiriki kikamilifu katika kufikia lengo la Kimataifa la watu asilimia 90 kujua hali zao za kiafya, Asilimia 90 wanaoishi na VVU kuwa wafuasi wa dawa za kupunguza makali na Asilimia 90 ya wanaotumia dawa waweze kufubaza makali ya ukimwi kufikia mwaka 2020.
Imetolewa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.