Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh George Mangalu katika ziara yake ya kutembelea taasisi za kidini na mashirika binafsi kwa lengo la kujionea ushiriki wake kwenye mapambano dhidi ya ukimwi na madawa ya kulevya
Amesema taasisi hizi na mashirika haya yanatakiwa kuwa mstari wa mbele yakisaidiana na Serikali katika kuhakikisha waliopata nafuu kutoka kwenye matumizi hayo ya madawa wanajenga misingi ya kujiamini, ikiwa ni pamoja na kupatiwa mikopo itakayowawezesha kuendelea na shughuli za ujasiriamali.
Kwa upande wake Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI Manispaa hiyo Bi.Rhobi Gwesso amesema, uelewa mkubwa unatakiwa kwa viongozi wa dini ili iwe rahisi kupeleka taarifa sahihi kwa jamii za jinsi ya kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Shirika lililotembelewa ni pamoja na BLUE CROSS lililoko Ununio na taasisi za kidini zilizopo oysterbay yote yakijishughulisha na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na UKIMWI.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.