Maafisa Ustawi wa Jamii wametakiwa kuzitolea taarifa kesi za watoto walio kwenye mazingira hatarishi na waliofanyiwa ukatili na kuziingiza katika mifumo wa DSMS na MVC Mis.
Rai hiyo ilitolewa Mei 2, 2024, na Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es salaam, Bwn. Elisha Nyamala, wakati akizindua mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa ustawi wa jamii wa Manispaa ya Kinondoni. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa DMDP Magomeni.
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Shirika la Global Child Advocates Tanzania, Bwn. Onesmo Itozya, aliwataka Maafisa hao kufuata Kanuni za kutoa taarifa za watoto walio kwenye makao ili kurahishia wadau wengine wanapofanya tathmini za kuwarudisha watoto hao wasipate shida.
Vilevile Maafisa walitakiwa wamiliki wa makao kuwashirikisha wadau mbalimbali na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kurahisisha taratibu za kuwatengamanisha watoto na familia zao.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.