Soko maarufu la nafaka na bidhaa nyingine la Tandale lililofikia asilimia 99 ya ujenzi, linatarajiwa kuanza kutumika Julai 30, 2024 baada ya kukamilika kwa taratibu za upangaji wafanyabiashara uliozingatia mahitaji ya kila mfanyabiashara na aina ya bidhaa wanazouza.
Afisa Biashara, Viwaanda na Uwekezaji wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Phillipo Mwakibete, Julai 29, 2024 akiwa sokoni hapo aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa, “Tunatarajia kuona wafanyabiashara wetu wakinufaika na fursa hii ya kuwa na soko la kisasa, ambalo litawawezesha kuuza bidhaa zao katika mazingira safi na salama.” Zaidi Wafanyabiashara 2000 wanatarajiwa kutumia soko hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, aliwataka wafanya biashara hao kuwa na subra wakati maboresho yakikamilika
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.