Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amewataka Watumishi wa Hospitali wa Wilaya ya Mabwepande kusimamia misingi ya Utumishi wa Umma ikiwemo Uzalendo, Utii, Uhodari, Weledi na juhudi katika kutoa hudumia za afya.
Ametoa rai hiyo Juni 3, 2024 alipokutana na Watumishi wa Hospitali hiyo na kuwaasa kuacha mambo yote yatakayojenga taswira mbaya katika Hospitali ya Wilaya, ikiwemo ulevi, lugha mbaya, madeni yaliyopitiliza, mavazi mabaya na uzembe kazini.
"Zingatieni nidhamu katika kazi na kuimarisha mshikamano baina yenu ili kuikuza Hospitali hii", amesema Mhe. Mtambule.
Vile vile, amewataka watumishi hao kusimamia ulinzi na usalama wa mali zote ndani na nje ya Hospitali ili kuendelea kurahisisha utolewaji wa huduma bora za kiafya.
Pia, Mkuu wa Wilaya huyo amewaomba kuwa wabunifu katika kutoa huduma na kutoa taarifa za kiafya kwa wananchi ili kuleta mafanikio ya Mabwepande na Kinondoni kwa ujumla.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.