Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, Januari 08, 2024 amewataka wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto wao ili wapate elimu iliyo bora na kufikia malengo yao.
Mhe. Mtambule ameyasema hayo akiwa katika ziara yake katika Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Muhalitani iliyopo Kata ya Tandale.
Alisema, "ili watoto wapate elimu iliyo bora yawapasa wazazi kushirikiana na walimu kusimamia vyema maadili ya watoto wao kwani elimu bora inahitaji nidhamu, bidii na kujituma."
Aidha, Mheshimiwa Mtambule alisema kuwa, wakati Serikali inatimiza majukumu ya kuandaa miundombinu, walimu na vitendea kazi vingine, wazazi na walezi pia wanatakiwa kutimiza majukumu yao ya msingi ikiwepo kutowaficha watoto wenye ulemavu.
Aliongeza kuwa, "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa fedha katika shule zote kwa mwaka huu wa masomo 2024. Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ili kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora.
Naye, Bi Agnes Stanley akiongea kwa niaba ya wazazi waliofika shuleni hapo ameishukuru Serikali na kuahidi kushirikiana na uongozi wa shule ili wafikie malengo ya kuwa na shule bora kwa Kata ya Tandale.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.