Akiwa katika Kata ya Makongo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Hanifa Suleiman Hamza, ametembelea Shule ya Msingi Makongo Juu kuona baadhi ya miundombinu ya Madarasa iliyoaribika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Alipokelewa na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Joseph Rwegasira, amempitisha Mkurugenzi huyo kujionea miundombinu iliyoaribika. Bi. Hanifa ametoa pole kwa Wananchi wa Kata hiyo.
"Kwa kweli juhudi za haraka zinaitajika kwa Shule hii, hata tuanze na madarasa machache kwasasa, tukijipanga na bajeti ijayo, haiwezekani shule jirani ya English medium watoto waendele kusoma halafu hii tuifunge. Ni jambo lisilowezekana". alisema Mkurugenzi Hanifa.
Naye Diwani wa Kata ya Makongo Mheshimiwa Joseph Rwegasira, amemshukuru sana Mkurugenzi kwa kuja kujionea hali ya Shule hiyo. Sambamba na hilo alimshukuru sana Mkurugenzi huyo kwa kuchukulia jambo hilo kwa uzito mkubwa sana.
"Nakushukuru sana Mkurugenzi kwa jitihada hizi na kuchukua hatua za haraka. Jambo hili umelipa uzito mkubwa, Wanamakongo tunashukuru".
Maboresho hayo yanatarajiwa kuanza katikati ya Mwezi Mei.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.