Diwani wa Kata ya Kigogo Mhe. Richard Mgana amewataka Wananchi kupaza sauti katika uibuaji wa maovu yanayotokea katika jamii badala ya kukaa kimya na kulindana.
Mhe. Mgana ameyasema hayo leo katika kikao cha ushiriki wa wanawake katika nafasi za kiuongozi na kiuchumi kilichofanyika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kigogo.
"Jamii zetu zimekuwa na kasumba ya kuyanyamazia maovu yanayotokea katika familia zetu hususani masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto, kwa minajili ya kulindana" ameongeza Mhe. Mgana.
Kadhalika, Mkurugenzi wa Shirika la wanawake katika jitihada za kimaendeleo (WAJIKI) Bi. Janeth Mawinza amewataka wazazi hususani wamama kupaza sauti katika ulinzi wa watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa matukio ya unyanyasaji katika jamii yetu.
"Mara kadhaa Wazazi tunafanya mambo ambayo watoto hawatakiwi kuyaona hadharani, kwa mfano shughuli zetu za kijamii zinazohusisha mambo ya watu wazima watoto wasione" amesema Bi. Janeth.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.