Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, ameziomba Mamlaka kufanya mapitio ya Sheria ya usimamizi wa biashara ya baa ili iendane na wakati.
Mheshimiwa Songoro alitoa rai hiyo Desemba 19, 2023 katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila na wamiliki wa Bar, Night club na Grocery. Kikao hicho kilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.
Mheshimiwa Songoro alisema kuwa, "kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo kwa sasa, kuna haja ya kufanya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 1968 ambayo inamtaka mmiliki wa baa afungue saa 12 jioni na kufunga saa 5 usiku kwani hali imebadilika sana sio kama zamani."
Hata hivyo, Mheshimiwa Songoro aliwataka wamiliki hao kuzingatia Sheria hiyo inayowaongoza kwa sasa.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Baa na Kumbi za Burudani Tanzania, Bw. Mponjoli Mwarabana, alisema kuwa kutokana na Mji wa Dar es Salaam kuwa ni wa kibiashara, kuna haja ya kubadilishwa kwa sheria hiyo ambayo itaongeza muda wa biashara na hatimaye kuchangia mapato kwa Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.