Ni kauli yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe alipokuwa akizungumza na Wamachinga wa eneo la Mwenge leo katika kikao kilichofanyika Mwenge Coca cola
Amesema Wamachinga walioko Mwenge tayari walikwisha pangwa kwa utaratibu uliokubalika hapo awali na kuwataka kila mmoja kutekeleza wajibu wake kwa kurudi eneo rasmi ili kuondokana na bugudha yoyote.
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha Wamachinga wanawekewa miundombinu rafiki itakayowawezesha kufanya kazi zao zinazowaingizia kipato bila bugudha yoyote.
"Hatukuja kufanya jambo jipya, Wamachinga wa Mwenge walikwisha pangwa, niwaombe ndugu zangu turejee kwenye maeneo yetu kabla ya tarehe 18 Oktoba, 2021". Amesema Mheshimiwa Gondwe.
Naye Mwenyekiti wa Wamachinga Taifa ndugu Lusinde alipokuwa akizungumza ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapanga Wamachinga katika maeneo rasmi ili waweze kufanya biashara zao kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Gondwe ameainisha maeneo yasiyotakiwa Wamachinga kufanya biashara zao kuwa ni maeneo ya mtaro na hifadhi ya barabara, maeneo ya wapita kwa miguu, mbele ya biashara ya mwenzako pamoja na sehemu za miundombinu ya umeme na DAWASCO.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na dawati la kuwapanga Wamachinga Wilaya ya Kinondoni, Afisa Biashara Wilaya, Afisa Habari Taifa na Mkoa, Mwenyekiti wa Wamachinga Taifa pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.