Ataja Tandale kuwa eneo la uzinduzi wa Kampeni ya Usafi
Asema Billioni 150 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja na Mto Msimbazi
Aunda Kamati Maalum ya Mazingira ya kuzuia Uharibifu wa Mazingira
Asisitiza Ulinzi na Usalama
Ampa OCD na Timu yake Wiki moja Kushughulikia KERO ya Uwanja wa Fisi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 22 Septemba, 2022 ameendelea na ziara yake ya kupita Jimbo hadi Jimbo ambapo leo alikuwa katika Jimbo la Kinondoni.
Akiwa Kinondoni Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Dar es Salaam inapaswa kuwa safi na ameanza kwa kuwapanga vema Wamachinga na sasa anaenda kuzindua kampeni ya usafi ambayo ataizindua katika Kata ya Tandale. "Wale wote walioanzisha magereji bubu yanayoweka magari barabarani waache mara moja". Alisisitiza RC Makalla.
Wakati huo huo RC Makalla amesema kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 150 ili kujenga mto Msimbazi ambapo mto huo unaenda kukabiliwa mwanzoni. Aidha, mto
Ng' ombe tayari Mkandarasi yuko eneo la kazi "site" na kazi inaendelea.
Kuhusu kuunda Kamati Maalum ya Mazingira Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuzuia waharibifu wa mazingira na wachimbaji wa michanga ovyo katika mito.
Hata hivyo Mhe. Makalla amewataka wananchi wote kuendelea kudumisha Ulinzi na Usalama kwa maendeleo ya Taifa letu sambamba na kuwafichua wahalifu wote.
Wakati huo huo Mhe. Mkuu wa Mkoa amempa muda wa jumai moja OCD na Timu yake kushughulikia KERO sugu ya Uwanja wa Fisi ili wananchi wakae kwa amani na utulivu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.