Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Februari 22, 2024 amezindua Nyumba za Walimu zenye thamani ya shilingi milioni tisini na moja katika Shule ya Sekondari Godwin Gondwe iliyopo Kata ya Kunduchi.
Akizindua Nyumba hizo Mhe. Chalamila amewataka Wanafunzi hao kusoma kwa bidii, "mnapaswa kusoma kwa bidii bila kujali wanaosema Shule za Kata, mana kuna kasumba hiyo".
Hizi Shule hazijaanza leo kuna wakati tulipata msaada kutoka Serikali ya Cuba tukajenga Shule kama hizi, watu wakasoma ma wakafaulu shule hizi hizi. Aliongeza kuwa zamani tulisoma mbali, kutoka hapa kwenda kusoma Kigoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule alisema hii ni dhamira ya Rais wetu kuboresha elimu. Kwa kuwepo Walimu hapa, ulinzi utaimarika katika Shule yetu. Aliongeza kuwa "tutajenga Nyumba nyingi zaidi, huu ni mwanzo". Nyumba nyingine zipo pale kijitonyama Sekondari. Tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutujali kwa miradi mingi sana katika Wilaya yetu.
Naye Meya wa Manispaa Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge aliongeza kuwa sisi Kinondoni tunamtendea haki Rais wetu na pia tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga mkoni na wewe Mkuu wetu wa Mkoa tunakushukuru kwa kutuongoza na kutusimamia. Leo hii nakupongeza kwa kuja kushuhudia na tunakuahidi tunaendela kuchapa kazi.
Upande wake Mwenyekiti wa Huduma za Uchumi, Afya na Elimu Mhe. Richard Mgana, Diwani wa Kata ya Kigogo kwa niaba ya Kamati yake amepongeza ujenzi wa Nyumba hizo "Kwa hili Tunamtendea haki Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Awaasa Wanafunzi waachane na makundi wasome, wajitume.
Mwisho Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Nuriath Rusheke ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suhulu Hassan kwa ujenzi huo wa Nyumba za Walimu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.