Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameutaka uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kusimamia vyema mchakato wa upatikanaji wa Viongozi waadilifu wa soko la Makumbusho ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika soko hilo.
RC Chalamila amesema hayo leo Agosti 16, 2023 wakati akiongea na wafanyabishara kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakumba wafanyabiashara wa soko hilo.
Aidha Mhe. Chalamila amekemea vikali uwepo wa madalali katika soko hilo ambao hupandisha bei za upangishaji wa fremu na meza, kuepuka rushwa, pia kuimarisha ulinzi shirikishi, na usafi wa soko pamoja na Viongozi wa mwanzo kutogombea tena nafasi za uongozi katika soko hilo wapishe Viongozi wapya.
Pia, Mkuu wa Mkoa huyo ameagiza TAKUKURU kuwakamata wale wote wanaohusika na uuzaji wa meza kwa bei ya juu wahojiwe na wakikutwa na hatia wapelekwe Mahakamani. Amewahakikishia wafanyabishara hao kuzimaliza changamoto zote katika soko hilo kwa kipindi kifupi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amesema soko hilo lina wafanyabishara takribani 883 na dhamira ya Manispaa ni kuboresha soko hilo, kupata uongozi imara wenye kutetea masilahi ya wafanyabishara na ndio maana tuliamua kuvunja uongozi wa mwanzo na sasa tuko katika kipindi cha mpito kupata uongozi mpya wa soko.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.