Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila ameagiza Wakala wa Maji na Mazingira Vijijini (RUWASA) kupeleka mashine za kuchimba visima vya maji katika Soko la Tandale kwa haraka ili kuharakisha uzinduzi wa soko hilo hivi karibuni.
Dkt. Nguvila alitoa tamko hilo Juni 07, 2024 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika soko la kimkakati la Tandale, ambalo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni. Ziara hiyo ililenga kukagua maandalizi ya mwisho ya soko hilo na kuhakikisha kuwa miundombinu ya soko hilo ipo tayari kwa ajili ya uzinduzi. "Nahitaji mashine za kuchimba visima ziwepo hapa ifikapo saa kumi na mbili jioni ya leo, na ikifika muda huo nitapita kuhakikisha kama mashine hizo zimefika hapa."
Ziara hiyo, iliwajumuisha maafisa mbalimbali wa serikali, viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, na wawakilishi wa wafanyabiashara. Dkt. Nguvila alipokelewa na viongozi wa soko na kuanza ziara ya kukagua miundombinu na huduma zitakazotolewa katika soko hilo jipya ikiwemo sehemu za kuhifadhi bidhaa pamoja maeneo ya biashara. Alionyesha kuridhika na maendeleo ya ujenzi na mipango iliyowekwa kuhakikisha soko linafanya kazi kwa ufanisi mara baada ya kuzinduliwa. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo, Dkt. Nguvila alisema,
"Nimefurahishwa sana na kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa soko hili la Tandale. Mradi wa soko utatoa manufaa kwa pande zote mbili ikiwemo Wananchi pamoja na Halmashauri ambapo ujenzi wa soko hili la kisasa la ghorofa unatarajiwa kuongeza nafasi za wafanyabiashara wengi wapatao 2055 kufanya biashara zao kwa usalama na unadhifu zaidi. Na pia kwa upande wa Halmashauri soko hili litasaidia Halmashauri kujiongezea mapato yake." Aidha, Dkt. Nguvila alitoa pendekezo la kutumia nishati salama katika mapishi ya vyakula vya biashara vitakavyouzwa ndani ya soko hilo.
"Katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhimiza matumizi ya nishati salama tunaondoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa hivyo tunatarajia soko hili kufungwa mifumo itakayowezesha matumizi ya gesi na hatutarajii kuona mama lishe na baba lishe wanatumia
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.