Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila, ameshauri Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kutoa motisha kwa Watumishi wanaofanya kazi vizuri ili kuleta ushindani baina ya Watumishi na tija kazini.
Dkt. Nguvila aliasema hayo katika kikao kazi baina yake na watumishi wa Manispaa Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani. Alisema, "wekeni utaratibu wa kutoa motisha ili kuleta ushindani kazini na zawadi zenye thamani kwa watumishi."
Aidha, Dkt. Nguvila aliendelea kusisitiza usimamiaji miradi, ukusanyaji mapato na kufanya kazi kwa weledi Ili kuendelea kuyaishi maneno ya Rais wetu kwa vitendo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.