Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo alipozuru katika hospitali ya Mwananyamala kujiridhisha na hatua za ujenzi wa jengo jipya la mama na mtoto linalojengwa na chuo cha MUST Mbeya lililohusisha uwekaji wa CT-scan na X ray limekamilika kwa kiwango kilichokusudiwa.
Amesema kuzuru kwake hapo ni katika kuhakikisha shughuli zinazotekelezwa na Serikali katika nyanja mbalimbali na kugusa wananchi zinakamilika kwa kusudi mahususi hasa ikizingatiwa yeye ndiye mwakilishi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwatumikia wananchi Wilayani kwake.
"Hakika ninawapongeza sana kwa ujenzi wa jengo hili lenye kiwango mahususi uliohusisha mtazamo wa mbali ulio chanya katika uwekaji wa vifaa muhimu, haya ndiyo mambo Serikali yetu inayataka, kuwa na ubunifu kama huu wa uwekaji wa CT Scan na X-ray katika ujenzi kwani uhitaji wake ni wa muhimu sana, huo ni uthubutu wa hali ya juu" Ameongeza Mh Chongolo.
Naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya hiyo Dr. Daniel Nkungu katika mazungumzo yake amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa uzalendo alionao katika ufuatiliaji wa miradi ya Serikali kwani kwa kuzuru kwake katika jengo hilo kunaamsha hamasa si tu ya utendaji kazi, bali umakini katika kuhakikisha miradi ya serikali inakamilika kwa tija iliyokusudiwa.
Imeandaliwa na
kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.