Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuongeza kasi na ubunifu katika ukusanyaji wa mapato ili kuharakisha ujenzi wa miradi mbalimbali. Mheshimiwa Chalamila ametoa kauli hiyo Juni 26, 2024 katika
kikao cha baraza la Madiwani la hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/2023 katika ukumbi wa Manispaa ta Kinondoni.
Akiongea katika baraza hilo Mkuu wa Mkoa amesema inahitajika ubunifu wa hali ta juu katika ukusanyaji wa mapato ambayo ndio nyenzo kubwa katika kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania. "Nafahamu Manispaa ya Kinondoni mmekua kinara kwa miaka kadhaa katika ukusanyaji mapato hivyo niwaombe muendelee kuchapa kazi na kuongeza ubufu wa ukusanyaji mapato hasa kwenye Masoko ambayo tumekua tukilega lega kwa kiasi kikubwa," amesema Mhe. Chalamila.
Mbali na hayo pia Mhe. Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kuwa na historia ya kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu (3) mfululizo ambapo amewataka kuendeleza utamaduni kwa kuzingatia maagizo na maelekezo ya CAG pamoja na kuzingatia ushauri unatolewa na wakaguzi wa ndani (Inernal Auditors).
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.