Kauli mbiu ya Maonesho ya Nane nane kwa mwaka 2017 inasema "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo, mifugo, na uvuvi ili kufikia uchumi wa Kati. "
Kuzalisha kwa tija maana yake ni kuzalisha kwa faida ukitumia eneo dogo,na mbinu za kisasa za Kilimo, gharama nafuu na kupata mazao mengi na yenye afya.
Unachotakiwa ni kuhakikisha unapata mbegu bora za mbogamboga na maandalizi mazuri ya kitalu ili kupata miche yenye afya.
Mf unataka kufanya kilimo cha mbogamboga ,hatua muhimu ya kwanza ni kuhakikisha unaandaa kitalu chako ,panda miche ikishachipua, ihamishie kwenye tuta kwa kufuata kanuni bora za Kilimo ambazo ni :kuweka mbolea ya kutosha ,nafasi kati ya mche na mche, palizi kwa wakati, na kutumia dawa unapoona dalili yeyote ya wadudu.
Hali kadhalika unatakiwa kupunguzia matawi ambayo hayaitajiki, kumwagilia kwa wakati na maji ya kutosha.
Thamani imeonekana kwa kuwa katika banda la Manispaa ya Kinondoni unakutana na wataalamu mbalimbali wa Kilimo na Mifugo.
Wataalamu hawa wanakueleza hatua kwa hatua jinsi ya kuandaa bustani yako eneo lako la nyumbani au popote pale, jinsi ya kutumia njia bora za kilimo, ukapata faida kubwa kwa muda mchache na kwa kutumia gharama nafuu Sana.
Tembela banda letu la Kinondoni uelimike, ukutane na mtaalamu wa kuandaa eneo kwa ajili ya bustani ya mbogamboga Bi. Lucresia Tarimo.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.