Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, akishiriki zoezi la Sensa kwa kuhesabiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Bi. Hanifa amekuwa ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza katika siku ya kwanza ya Sensa ya watu na makazi iliyoanza leo Agosti 23, 2022 nchini kote.
Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Zoezi la Sensa ya watu na makazi linaendelea kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 23 hadi 29 Agosti, 2022.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.