Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na Maafisa Ugani wa Kata ya Bunju katika ziara yake aliyoifanya leo.
Amesema Maafisa ugani, watendaji wa Kata na Mitaa katika maeneo yao wanatakiwa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo ili kero za wananchi zinazowakabili zitatuliwe kwa ufanisi, umakini, na usawa utakaoleta tija iliyokusudiwa.
"Kutenda haki kunajengwa kwa kutimiza wajibu, nilazima muwe wasimamizi wajumla wa shughuli za Serikali katika maeneo yenu, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma stahiki kwa wananchi" Amesisitiza Mh.Chongolo.
Akisoma taarifa za Kata ya Bunju kwa Mkuu wa Wilaya, Mtendaji wa Kata hiyo Bw.Ibrahim Mabewa amesema Kata yake inamitaa 6, ambayo ni Bunju A, Mkoani, Dovya, Kilungule, Boko, na Basihaya na idadi ya watu kuwa takribani 63,248, na hii ni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
Aidha amezitaja changamoto zinazoikabili Kata hiyo ya Bunju kuwa ni Uchimbaji wa kokoto na vifusi, Uchimbaji holela wa mchanga maeneo ya Nyakasangwe, Dampo la taka kuwa mbali na mrundikano wa takataka.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameupongeza uongozi mzima wa Halmashauri kwa ufaulu wa asilimia 95.7, matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018, uliopelekea Kinondoni kuwa ya kwanza kimkoa, na ya tatu kitaifa.
Katika ziara yake hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea maeneo ya shule ya msingi Mkoani, soko la Bunju A, mifereji ya Basi haya, na baadae kufanya mkutano wa hadhara na wananchi katika viwanja vya shule ya Bunju, kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.