Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh Alli Hapi ametoa mwezi mmoja kwa shule zote za Msingi na Sekondari katika Manispaa yake, kuwa na waalimu walezi wa kike na wakiume watakaokuwa na jukumu la kuwasikiliza,kuwalea na kuwasaidia watoto hao, wanapokuwa katika mazingira hatarishi kwa maisha na afya zao mashuleni.
Ametoa agizo hilo leo, alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ukarabati wa majengo ya shule ya Msingi Boko, kwa ufadhili kutoka Asasi ya kiraia ya "TIME TO HELP", kushirikiana na wananchi pamoja na Serikali.
Amesema waalimu hao walezi wawe na ushirikiano na dawati la jinsia la jeshi la polisi, ili iwe rahisi kutoa taarifa pale inapoonekana mwanafunzi ametendewa vitendo viovu.
"Afisa Elimu Msingi na Sekondari, ninawaagiza kuwepo kwa waalimu walezi kwa watoto wakike na wakiume, na waalimu hao wawe wenye upendo, subira, uvumilivu na wepesi kusikiliza, na pia wawe na ushirikiano na dawati la jinsia la jeshi la polisi, ili tuweze kuwalinda watoto wetu dhidi ya vitendo viovu "Amesema Hapi.
Naye Afisa Elimu msingi Manispaa hiyo Ndg Kiduma Mageni ameahidi kutekeleza swala hilo ,ili watoto wetu wawe katika mikono salama itakayowaepusha na utendewaji wa vitendo viovu.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.