Hali hiyo imebainika wakati Naibu waziri wa Ajira, Kazi na Vijana Mhe Patrobas Katambi alipofanya ziara kutembelea vikundi vya vijana vilivyokopeshwa vitendea kazi vinavyowasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali.
Amesema kwa kumpatia kijana kifaa ni uamuzi mzuri unaomwepusha kutumia fedha kinyume na utaratibu na kumuondolea tamaa za matumizi mabovu hali inayompelekea kutokukamilisha malengo mahususi
"Niwapongeze pia kwa ajili ya eneo hili la utoaji mikopo, Kinondoni mmeweza kwa kuhakikisha mnasimamia taratibu, Sheria, kanuni na miongozo invyoelekeza kuhusiana na suala hili ngazi kwa ngazi kwani mchakato unaanzia ngazi ya chini hali inayopelekea kupata watu sahihi zaidi wa kuwapatia fedha hizi" Ameongeza Mhe Katambi
Akiwa Katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha EZEMA, Naibu waziri huyo ameridhishwa na bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo na kuahidi kuwa balozi wa bidhaa hizo popote atakapokwenda.
Aidha amewataka vijana wa kiume kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hii kwani takwimu za Sasa zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaojitokeza kuchukua mikopo ni kubwa zaidi ukilinganisha na vijana.
Awali akitoa Taarifa ya utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Kinondoni, Bi Halima Kahema amesema wameamua sasa kukopesha vifaa, na viwanda vidogo ili kuwawezesha wajasiriamali kwenda moja kwa moja kwenye uzalishaji.
Kadhalika amebainisha kuwa kwa mwaka 2017 wamefanikiwa kukopesha zaidi ya vikundi 5000 na kuwa kwa mwaka huu wa fedha wameshatoa mikopo kwa vikundi 202 ambapo wamepata kiasi cha shilingi Bil 1.3 .
Naibu waziri akiwa amembatana na Kamishna wa Kazi nchini ametembelea kikundi cha kutengeneza juisi cha Emitote na kikundi cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha EZEMA.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.