Akizindua miradi hiyo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ndugu Charles Kabeho amesema miradi aliyoizindua, aliyoiwekea jiwe la msingi na kukagua ikawe chachu ya maendeleo kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda wenye lengo la kumkwamua mwananchi wakawaida kabisa na mwenye kipato cha chini.
Awali akifafanua ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 usemao "Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu" ndugu Kabeho amesema Wilaya ya Kinondoni imeonesha dhamira ya dhati juu ya utekelezaji wa kauli mbiu hiyo kwa kuibua mradi wa shule ya sekondari kidato cha tano na cha sita Tumaini mabwe uliowekewa jiwe la msingi utakaosaidia wanafunzi wa kike kusoma bila bugudha.
Akiupokea Mwenge huo kutoka Kigamboni, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi amesema Wilaya yake Mwenge utakimbizwa Km 83.3, na kuzindua, kuweka jiwe la msingi na kukagua miradi saba
Ameitaja miradi hiyo Kuwa ni kituo cha kutoa mafunzo ya kujikinga na maambukizi ya VVU na dawa za kulevya (MEFADA), Matengenezo maalum ya barabara ya CCBRT, na Mradi wa mazingira (shamba la miti ya mitiki),
Miradi mingine ni Mradi wa Ufugaji wa kuku (KROILER) Mabwepande, Ujenzi wa wa madarasa 4, Maabara 3, Bweni 1, Nyumba za walimu 4, Ofisini ya walimu 1, Bwalo 1, Ukuta, vifaa vya shule, Vitanda, Magodoro, Umeme, Choo na kuingiza maji shule mpya ya kidato cha tano Mabwe Tumain Girls na Ujenzi wa soko la Tegeta Nyuki.
Katika hatua nyingine Mkimbiza Mwenge Kitaifa ndugu Charles Kabeho alipata fursa ya kukagua vikundi vya ujasiriamali, kushuhudia wananchi wakipima afya zao, na kuona ushuhuda ukitolewa kuhusiana na athari za madawa ya kulevya.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.