Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeingia Wilayani Kinondoni, Mei, 11 2024 kutokea Kigamboni na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule katika viwanja vya shule ya msingi Mapinduzi iliyopo katika Kata ya Kigogo.
Ukiwa Kinondoni Mwenge wa Uhuru utapitia miradi nane iliyopo katika Kata nane za Kigogo, Kinondoni, Wazo, Mabwepande, Kijitonyama, Kunduchi, Makongo na Kawe yenye jumla ya Shilingi 75,922,104,212/=.
Miongoni mwa miradi hiyo ni Mradi wa Klabu ya Wapinga Rushwa ulipo katika Shule ya Msingi Mapinduzi ambayo imegharimu kiasi cha Shilingi 500,000/= katika kata ya Kigogo.
Mradi mwingine ni jengo moja la ghorofa lenye wodi ya wazazi, sehemu ya upasuaji uliopo Kata ya Kinondoni wenye Shilingi 1,359,310,764.12/=
Aidha, Mwenge utapitia ujenzi wa barabara ya nyota Njema uliopo katika Kata ya Kunduchi yenye urefu wa km 1.4 kwa kiwango cha lami uliogharimu kiasi cha Shilingi 1,830,401,197.04/=
Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) na Huduma za Afya ya Uzazi (RCH) Zahanani ya Mabwepande uliopo katika Kata ya Mabwepande, uliogharimu kiasi cha Shilingi 268,981,424.34
Kikundi Cha Vijana cha Wauza Dawa (Pharmacy) kilichopo katika Kata ya Kijitonyama kilichogharimu kiasi cha Shilingi 50,000,000/=
Kituo cha Utengamao (Rehabilitation Center) kwa watu wenye ulemavu Antonio Verna-Kawe pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa usambazaji maji kati ya Makongona Mji wa Bagamoyo kupitia DAWASA uliogharimu kiasi cha Shilingi 268,981,424/=
Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba 24 vya madarasa (ghorofa), matundu 48 ya vyoo,Vyumba 3 vya maabara, maktaba 1, jengo la Utawala na kisima cha maji chini ya ardhi katika shule ya Sekondari Changanyikeni iliyopo Kata ya Makongo ambao umegharimu kiasi cha Shilingi 678,998,425.00/=
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.