Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema uimara wa Muungano wetu unategemea uwepo wa vijana imara na wenye uchungu na Taifa lao.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akilihutubia taifa juu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Taifa la Tanzania.
"Uimara wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Taifa la Tanzania upo katika mikono ya vijana, hivyo vijana wanatakiwa kuwa imara na uchungu wa Taifa lao katika kuuenzi Muungano huu ulioasisiwa na viongozi wetu Mwl. Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume," alisemaa Dkt. Samia.
Pia, Mhe. Rais Dkt. Samia alisema kuwa Muungano huo umeleta mafanikio makubwa katika nyanja ya Uchumi, Kijamii na Kidemokrasia hivyo ikumbukwe kwamba Muungano unahitajika leo kama tulivyouhitaji mwaka 1964.
"Kila mmoja ana uhuru na jukumu la kulinda mipaka ya Taifa letu na kujua kwamba mlinzi wa kwanza wa kulinda Muungano ni Mwananchi mwenyewe".
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.