Ni kauli yake Mh Phares Lupomo,Diwani Kata ya Mbezi juu alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yenye kauli mbiu isemayo "Kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, tusimwache nyuma mtoto " yaliyofanyika katika kata yake ya Mbezi juu, kwa kuwahusisha watoto katika michezo mbalimbali .
Amesema, lengo la maadhimisho hayo pamoja na vitu vingine ni kumuunganisha, kumchochea na kumkumbusha mzazi wajibu wake kwa mtoto ambaye ndiye taifa tegemezi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda.
"Tulipofikia hapa Kama viongozi tunatakiwa kukumbuka kwamba nasi pia tulikuwa watoto hivyo nawaomba wadau wote tuungane pamoja kuwaandalia kesho njema watoto wetu kwa kujali, kulinda na kuwapa stahiki zao za msingi leo" .Amesema Mh Phares.
Naye Afisa Maendeleo ya jamii wa Kata hiyo Bi Julieth J Nzugika amewasihi wazazi na wanajamii kwa ujumla kuzingatia ,kuheshimu na kuzidumisha haki za watoto ili waweze kufikia ndoto zao.
Amezitaja haki hizo kuwa ni kulindwa, kupewa elimu bora, kuwa na malazi salama na kusikilizwa, ambavyo ndio msingi imara utakaomwezesha mtoto kujitambua na kujithamini kufikia ndoto anayoitazamia kwa maisha ya sasa na ya baadae.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.