MTAA wa Madale uliopo Kata ya Wazo, Manispaa ya Kinondoni, umepata eneo lake la nyama choma maarufu Kama FLAMINGO.
Eneo hilo lenye ukubwa hekta 3.6 sawa ekari 22 lipo Mtaa wa Madale ambapo huduma za mbuzi choma, mbuzi hai, machinjio ya mbuzi na vinywaji vinapatikana.
Mwenyekiti wa mnada huo, Bw. John Morro, mnada huu unahudumia mitaa ya Mivumoni, Mbopo, Wazo, Nyakasangwe, Tegeta, Salasala na mitaa mingine ya jirani ambao kwa sasa unawafanya biashara ndogo ndogo wapatao 300.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa, "Mnada unaojulikana kama wa Madale haupo eneo hilo, bali upo Wilaya ya Ubungo Kata ya Goba na hivyo haustahili kuitwa mnada wa Madale. Mnada wa Madale ndiyo huu tuliouanzisha na ambao leo sisi wana Madale na uongozi wa Manispaa tumefanya usafi."
Mnada huu, amesema, "tunapenda kutumia jina la FLAMINGO MADALE KWA KAWAWA maarufu Kama "Mbuzi Kunoga." Amesema kuwa Mzee KAWAWA ndiye mwanzilishi wa Madale ambayo ipo Manispaa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.