HALMASHAURI YA MANIPAA YA KINONDONI
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Kawe Sitta leo amepokea ujumbe kutoka Hong Kong Polytechnic University ( HKPU) ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi utakaosaidia kuimarisha uwezo wa Taasisi zetu mbili za Kilimo Malolo na ufundi Wazo katika kutoa taaluma bora zaidi na hatimaye kuweza kufikia malengo ya manispaa ya Kuwawezesha Wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na vijana kunufaika na Tekinolojia itakayotolewa katika vyuo hivyo.
Ujumbe huo wa Chuo Kikuu cha HKPU Umeongozwa na Ndugu CHAN Stephen ,Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa njia ya kujitolea na Profesa Grace Ngai ,Mkuu wa Idara ya Komputa ambapo Mstahiki Meya wa Kinondoni Pamoja na Mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Tanzania na kuwashukuru kwa nia na dhamira ya Chuo hicho kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi na vyuo vya Tanzania ikiwemo Kituo cha Mafunzo Malolo na Chuo cha Ufundi Wazo kinachotarajia kufunguliwa mwezi Februari mwaka huu 2019.
Akizungumza na Ujumbe huo Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Kawe Sitta, amewataka Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni hususani wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na Vijana inayotolewa na Manispaa kujiunga kwa mafunzo mbalimbali ya ufundi katikia vituo hivyo viwili ili waweze kunufaika na ushirikiano wa Manispaa ya Kinondoni na chuo hiki Maarufu cha Hong Kong Polytechnic University.
Kiongozi wa Ujumbe huo Ndugu CHAN Stephen Mkuu wa Idara ya mafunzo kwa njia ya kujitolea, katika mazungumzo yake amesema kuwa ziara yake hapa Nchini Tanzania inatokana na Fursa zilizopo za kutoa Huduma za Kijamii katika Nyanja za Kiteknolojia na ufundi kama wanavyofanya Nchini Rwanda hivyo ujio wake ni mwanzo mpya wa Mashirikiano katika nyanya hizo .Pia amewawakikishia Watanzania Kunufaika na Ushirikiano wa Kihistoria uliopo kati ya Tanzania na China.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, MAWASILIANO ITIFAKI NA MAHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.