Wanafunzi wametakiwa kutokunywa vinywaji vyenye kemikali, badala yake wanywe maziwa na kula vyakula vilivyopo kwenye makundi matano.
Wito huo ulitolewa Aprili 15, 2024 na Afisa Mifugo wa Manispaa y Kinondoni, Bi. Malkia Mbilinyi, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kwa nyakati tofauti kuhusiana na masuala ya Lishe.
Alisema, "Vijana jengeni tabia ya kunywa maziwa kwa ajili ya kujiongezea Protini na kula makundi matano ya vyakula. Msitumie vinywaji vyenye Kemikali kama 'energy' wala soda."
Aidha, Bi.Malkia aliwasihi walimu katika shule hizo kuanzisha miradi ya ufugaji wa wanyama wadogo wadogo wanaoliwa katika mazingira ya shule na nyumbani ili kurahisisha upatikanaji wa vyakula vitokanavyo vya wanyama. Shule za msingi zilizotembelewa ni Mwenge, Shekilango, Mapambano na Kawe Kids Daycare, wakati Shule za Sekondari ni Hananasifi na Abbas Tarimba. Sambamba na elimu ya Lishe pia wanafunzi wa Shule hizo walipokea maziwa ili kuwapa hamasa ya kuendelea kutumia zao la maziwa kama chanzo cha protini mwilini.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.