Wanawake wametakiwa kutokatishwa au kukataa tamaa na kukataa kejeli kutoka kwa makundi mengine ndani ya jamii zao.
Badala yake wametakiwa waongeze juhudi katika kutafuta nafasi za uongozi wa kisiasa na kujiinua kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake.
Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 8, 2024 katika Viwanja vya Mji Mwema Wilayani Kigamboni.
Mheshimiwa Chalamila alisema, "Niwaombe Wanawake msikubali kukatishwa tamaa, ikataeni kejeli, kataeni udhalimu bali muongeze juhudi huku mkitetea haki."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.