Serikali imeombwa kuwafuatilia watu wasio Madaktari wanaowazuia wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuendelea kutumia dawa zinazofubaza virusi hivyo.
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa TAPOT, Mwl. Hellen Thomas Masao, wakati akiwasilisha salamu kwa niaba ya wadau wa Mapambano dhidi ya UKIMWI.
Manispaa ya Kinondoni, imeadhimisha siku ya UKIMWI kiwilaya leo katika Kata ya Makumbusho ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Joseph Rwegasira.
Alisema, "wapo wachungaji ambao wanaowazuia watu kutumika ARV kwamba wanawaombea kwa mikono kichwani. Jambo hili si sahihi. Tusiingilie fani za Madaktari."
Mwl. Masao amewashauri waishio na virusi kusali huku wakitumia dawa bila kuziacha.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.