Diwani wa Kata ya Mzimuni, Mheshimiwa Manfredy Lyoto, amesisitiza umuhimu wa ulaji wa mlo bora na vyakula vya asili kwa ajili ya kuboresha afya na kinga dhidi ya magonjwa.
Mheshimiwa Lyoto aliyasema hayo Aprili, 3 2024 wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Lishe kwa Watendaji wa Kata za Mzimuni, Kigogo, Magomeni na Ndugumbi yaliyofanyika katika ofisi ya Kata ya Mzimuni.
Alisema, "Mlo bora husaidia ubongo kufanya kazi vizuri na kumuweka mtu kwenye mstari mzuri wa maisha yake."
Diwani huyo pia ameipongeza serikali kwa mpango wake wa lishe na ameitaka kuwa endelevu ili jamii iweze kujifunza na kuzingatia lishe bora kwa vitendo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.