Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi ameongoza mbio za polepole pamoja na matembezi ya haraka yenye umbali wa km 4.7 katika tamasha la mazoezi na michezo kwa watumishi na wananchi wa Manispaa ya Kinondoni.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu "FANYA MAZOEZI WEKEZA KATIKA AFYA "limefanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Posta Kijitonyama kuanzia saa 12:30 asubuhi mpaka saa 3:00 na kuhudhuriwa na watu wengi.
Akizungumnza katika Tamasha hilo Hapi amesema ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kuhusiana na kuhamasisha watumishi na wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara kama sehemu ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Shinikizo la damu, Kisukari na Magonjwa ya Moyo.
Amesema ni vema kujenga Utamaduni wa kufanya mazoezi, kuyaishi mazoezi, kuyashika mazoezi, kujituma katika mazoezi, na pia tudumu katika mazoezi, kwani kwa kufanya hivyo kutaweza si tu kupunguza sumu mwilini, bali pia ni kuwa na afya bora na iliyoimarika.
Katika hatua nyingine ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuandaa "Corporate Jogging" kama sehemu ya kuwaleta pamoja taasis mbalimbali zilizoko Kinondoni ili nao pia wajenge utaratibu wa Kufanya Mazoezi.
Shughuli zilizofanyika katika tamasha hili ni pamoja na matembezi ya haraka, mbio za pole pole, mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.