AAHIDI KUTOA TSH MILIONI MIA MOJA KUKAMILISHA UJENZI ZAHANATI YA BONDE LA MPUNGA .
Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli amefanya ziara katika Manispaa yake kukagua miradi inayotekelezwa katika sekta ya afya ili kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilizofikiwa,ikiwa ni pamoja na kutathmini thamani ya fedha inayoendana na mradi.
Pia Mkurugenzi huyo katika ziara yake hiyo ameahidi kutoa kiasi cha tsh milioni miamoja ili kukamilisha kwa haraka ujenzi wa Zahanati ya bonde la mpunga iliyoko Kata ya msasani, inayojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo .
Ziara hiyo imefanyika leo ambapo Mkurugenzi huyo akiambatana na wakuu wa idara na vitengo amefanikiwa kuongea na wananchi pamoja na wauguzi ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa huduma katika sekta ya Afya na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi.
Akiongea mara baada ya ziara hiyo, Kagurumjuli amesema wakati umefika sasa wa kufanya kazi kwa vitendo na kuwatumikia wananchi wanaohitaji huduma zilizo sahihi na kwa wakati.
Amesema sekta ya afya ni muhimu sana hivyo inahitaji kuboreshwa ili iweze kutoa huduma kwa maisha ya mwanadamu na niwajibu wake Kama Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, kujiridhisha kwa huduma zitolewazo pamoja na utekelezaji wa miradi ya sekta hiyo unaoridhisha na unaoendana na viwango na ubora uliokusudiwa.
Aidha amewahakikishia wananchi kuboresha majengo yote yaliyochakaa, kukamilisha miradi yote iliyosimama, kuzipatia samani za ofisi maeneo yote yenye uhitaji huo ili kuondokana na adha wanayoipata wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo Kata ya Tandale, Msasani, Bunju, Mabwepande, wazo, Kunduchi na Kigogo.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.