Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi.Theresia Kyara, leo ametiliana saini mikataba ya utendaji kazi na Maafisa Elimu Kata, Walimu Wakuu na Watumishi wa Idara ya Elimu Msingi.
Utiaji saini huo umefanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo amewataka kutekeleza mkataba huo wenye lengo la kuinua zaidi ufaulu kwa wanafunzi.
Amesema malengo 17 waliyokubaliana lazima yatekelezwe. Mojawapo ya lengo ni kuhakikisha wanafunzi wa darasa la tatu wanaelewa na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiingereza.
Kwa upande wao, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wamesema malengo hayo yanatekelezeka.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.