Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo mara baada ya kutembelea ujenzi wa soko hilo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi Kata kwa Kata na kubaini kuwa kasi ya ujenzi ni ndogo na idadi ya vibarua waliopo site hairidhishi.
Amesema mkandarasi NAMIS CORPORATE anayejenga Soko hilo anatakiwa kuongeza nguvu kazi na kujenga usiku na mchana ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na ulete tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Kila mradi unamuda wake wa ujenzi, na mara nyingi muda unazingatia ubora, thamani na matokeo yatakayopatikana kwa mradi huo kukamilika, sasa mkandarasi unapochelewesha, thamani ya mradi kwanza inashuka, lakini pia unapoteza Imani kwa wananchi watumiaji wake, hivyo nakutaka wewe NAMIS CORPORATE hakikisha unafanya jitihada za kukamilisha huu mradi wa SOKO kwa wakati na kwa ubora na thamani iliyokusudiwa" Ameongeza Chongolo.
Mradi huo unaogharimu Bill 8.7 hadi kukamilika kwake unahusisha ujenzi wa vizimba 956, maeneo ya kupakilia na kushushia mizigo, maegesho 60 ndani ya jengo na maegesho 19 nje ya jengo ulianza mwezi Agosti 2019 na kutarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.
Awali Mkuu huyo wa Wilaya katika muendelezo wa ziara yake hiyo ya kikazi Kata kwa Kata alifanikiwa kusikiliza kero 32 kutoka kwa wakazi wa Tandale na kuzitafutia ufumbuzi.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.