Miradi ya elimu yenye thamani ya shilingi milioni 188, inayohusisha uchimbaji wa kisima, ujenzi na ukarabati wa madarasa, pamoja na ununuzi wa samani katika shule ya Msingi Boko imezinduliwa leo kwa kukata utepe na kuweka jiwe la msingi.
Akizindua miradi hiyo iliyotekelezwa kwa nguvu za wananchi, Serikali pamoja na Asasi ya Kiraia iitwayo "TIME TO HELP", Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amesema uzinduzi huu ni kiashiria tosha cha ushirikiano mzuri kati ya wanachi, serikali na wadau katika kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinatatuliwa kwa kiwango kikubwa.
"Pembe tatu ya ushirikiano ndio siri kubwa ya mafanikio katika sekta ya elimu, Serikali inaendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyopo katika sekta hii ya elimu, ili yaendane sambamba na ongezeko la wanafunzi, tunachojifunza hapa ni kwamba kwa kushirikiana tunao uwezo mkubwa wa kutatua changamoto "Amesisitiza Hapi.
Naye Afisa Elimu Msingi Manispaa hiyo Ndg Kiduma Mageni amewashukuru wanachi pamoja na Asasi ya "TIME TO HELP " kwa ukarabati huo utakaowezesha idadi kubwa ya wanafunzi kupata mahali sahihi pa kusomea.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, mwalimu Mkuu wa shule ya Boko Ndg Andrew Joseph, amesema shule yake inajumla ya wanafunzi 2289, na inazo changamoto ambazo ni ukosefu wa uzio pamoja na tatizo la mafuriko.
Uzinduzi huo umefanyika kwa vyumba vya madarasa sita vilivyojengwa na serikali kwa kishirikiana na nguvu za wananchi, na ukarabati wa majengo mawili, pamoja na kisima cha maji kutoka Asasi ya kiraia iitwayo "TIME TO HELP "
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.