Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetenga kiasi cha shilingi Milioni 300 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya ufukwe wa Coco, ikiwemo ujenzi wa maegesho ya magari ili kutatua changamoto za kiafya na usalama.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro Mnyonge, aliyasema hayo Aprili 18, 2024 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ya kukagua eneo la ufukwe huo.
Alisema, "katika bajeti tumetenga kiasi cha Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya kuboresha eneo la kuegesha magari. Awamu ijayo, tutaendelea tena kuboresha eneo jingine."
Hata hivyo, Mheshimiwa Chalamila aliushauri uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuwashirikisha Wafanyabiashara wakubwa wa eneo hilo kuchangia uboreshaji wa miundombinu kwenye ufukwe huo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.