Diwani wa Kata ya Mikocheni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Rehema Mandingo azindua kampeni ya usafi wa mazingira na nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuwawezesha Wanawake kuachana na matumizi ya Kuni na Mkaa.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo Aprili 20, 2024 Mtaa wa Michungwani Kata ya Mikocheni ikiwa ni moja ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suhulu Hassan katika kampeni yake ya usafi wa mazingira na nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko ya gesi kwa baadhi ya akinamama wa Kata hiyo.
"Binafsi nimewiwa kuanziasha kampeni hii ikiwa ni moja ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kutokana na jitihada anazozifanya za kuwawezesha Wanawake katika masuala mbalimbali ikiwepo kumtua mama mzigo wa kuni na mkaa kichwani," amesema Mhe. Mandingo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.