Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert John Chalamila ameitaka miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iwe ni chachu ya kuondoa vikwazo vya biashara na kukuza mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo.
Alitoa kauli hiyo Aprili 22, 2024 alipoongoza Dua na Sala ya kuliombea Taifa ikiwa ni kuzindua Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano iliyofanyika Manispaa ya Kinondoni.
Mhe. Chalamila amesema, "Wafanyabiashara wapewe Uhuru wa kufanya shughuli zao kwa masaa 24 ili kupata muda wa kutosha kujiongezea kipato na kukidhi mahitaji yao sambamba na kuongeza mapato ya nchi".
Aliongeza kuwa baadhi ya viongozi waache kuweka vikwazo kwenye baadhi ya biashara sambamba na kuzuia utoaji na upokeaji wa rushwa.
Mhe. Chalamila amesisitiza kuwa, maendeleo yaliyofanyika katika miaka 60 ya Muungano yawe ni chachu ya mafanikio. "Uwepo wa mwendokasi iwe ni chachu ya kukuza biashara zetu kwa kufika haraka maeneo ya biashara".
Aidha, Mhe. Chalamila amewataka wana Kinondoni kuona jinsi Serikali ilivyopanua uwanja wa elimu, uwekezaji na Uhusiano wa Kimataifa kama chachu ya kukua kiuchumi kwa kutumia fursa zilizopo kwa kuacha kulalamika, kudumisha umoja na kuendelea kufurahia matunda ya Muungano huo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.