NI KUFUATIA MKUTANO ALIOUITISHA LEO MKUU WA WILAYA HIYO MH ALLI HAPI
Wakazi wa Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kuishi bila hofu kufuatia kumalizika Kwa mgogoro uliokiwepo mahali hapo kwa muda mrefu.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi leo alipofanya kikao na wakazi wa eneo hilo
Amewahakikishia wakazi wa Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi kuwa wakati umefika kwa hofu yao ya kuondolewa katika maeneo hayo kuisha na kwamba hawataondolewa tena.
Amesema biashara ya kesi sasa mwisho na, wananchi wabaki kama walivyo.
Katika hatua nyingine Manispaa imetakiwa kufanya upimaji wa eneo hilo na kwamba kutakuwa na barabara, maeneo ya michezo ,shule na huduma nyingine za kijamii.
Amewataka wakazi hao kutoa ushirikiano wakati wa wataalamu Wa Manispaa wanafanya upimaji
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.