Ushauri huo umetolewa Septemba 10, 2024 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo ilipotembelea Mradi wa Shule ya Msingi Richard Mgana iliyopo Kata ya Kigogo.
Awali, Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Husna Juma, imeipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa ujenzi wa Shule hiyo Mfumo wa Ghorofa ingawa Fedha ililetwa kujenga Madarasa ya msambao.
"Kinondoni ilifanya maamuzi sahihi yanayotakiwa kuigwa na pia sisi kama kamati tumepata kitu Cha kujifunza" amesema Mhe. Husna.
Kadhalika, Mhe Husna ametoa Rai kwa Serikali kuangalia mahitaji stahiki katika ugawaji wa Fedha za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kulingana na maeneo husika, akitolea mfano Ujenzi wa Shule ya Richard Mgana ambayo kama siyo jitihada za dhati zilizochukuliwa na Manispaa isingejengwa kwakuwa Fedha iliyoletwa haikuendana na eneo husika.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.