Watumishi wa Manispaa 85 wa Halmashauri ya Kinondoni ya Kinondoni wamepatiwa mafunzo kazi ya Mfumo mpya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma wa Kielekroniki (National e-Procurement System of Tanzania - NeST) yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 26-28 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa TEHAMA wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Frederick Mhagama amesema lengo la mfumo huo ni kuwezesha Halmashauri na Taasisi za Kiserikali kuandaa mahitaji na kufanya manunuzi Kieletroniki kwenye taasisi husika.
Ameongeza kuwa, mfumo huo utarahisisha manunuzi na kupelekea yafanyike kwa wakati, manunuzi yatafanyika kwa uwazi, ushindani, usawa na pia utasaidia Halmashauri kufanya manunuzi kulingana na thamani ya fedha.
"Mfumo huu utasaidia udhibiti mzuri wa shughuli za ununuzi, kupata bidhaa zenye ubora na kwa gharama inayotakiwa". Ameongeza Bw. Mhagama.
Aidha, Bi. Neema Chambika, Afisa Ugavi wa Manispaa ya Kinondoni ameongeza kuwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni watarajie kupokea manunuzi kwa wakati na kupata ushirikiano wa kutosha kuhusiana na elimu ya mfumo huo.
Ameongeza kuwa, "Watumishi wameonyesha ushirikiano na utayari katika kujifunza na uelewa ni mkubwa na kadri manunuzi yanavyoendelea elimu itaongezeka kwa kila mmoja juu ya mfumo huo".
Vile vile, Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Ezra Ngereza ameongeza kuwa mfumo huo una manufaa makubwa kwa kuwa taratibu za manunuzi zitafanyika kwa uwazi na kwa wakati.
Mfumo wa NeST unapatikana kwa kupitia anuani: https://nest.go.tz
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.