Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, amesema kuwa mchango wa chakula kwa wanafunzi shuleni siyo jambo la hiari ni lazima.
Akizungumza Februari 23, 2024 katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi kwa kuongeza kiwango cha ufaulu, Mheshimiwa Mtambule aliwaomba walimu kuendelea kuhimiza wazazi kuchangia chakula kwa wanafunzi .
Mkuu huyo wa Wilaya alieleza kuwa, "lishe huongeza afya ya akili kwa Wanafunzi jambo ambalo litaimarisha ufaulu na kwamba,
Mchango wa chakula ni lazima sio hiyari." Aliwataka Walimu kuchangisha michango iliyo na kibali ili kuondoa mtafaruku.
Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, kuhusu lishe bora shuleni aliwaagiza Walimu kusimamia usafi na chakula katika shule na kuepuka mwanafunzi kupewa chakula cha aina moja kwani lishe bora hujenga afya ya akili ya mtoto.
Alisema, "Lishe ni agenda ya Taifa na nisingependa kuona Kinondoni tunakua nyuma." Alihimiza Maafisa Kilimo kutembelea shuleni kwa ajili kutoa elimu ya kilimo cha mboga mboga.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.