Kulingana na uwanzishwaji wa mpango wa chakula Mashuleni unaotekelezwa hivi sasa unaowataka Wanafunzi kula Shuleni, kumekuwepo na changamoto ya mazingira ya kuandalia chakula kwa baadhi ya Shule hivyo Kamati ya Lishe Manispaa ya Kinondoni imependekeza mazingira ya kuandalia chakula Mashuleni yaboreshwe.
Hayo yamesemwa Mei 22, 2024 kwenye kikao cha tathmini ya lishe ya robo ya tatu ya mwaka na Afisa Lishe wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Emiliana Sumaye kilichokutana kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa lishe ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
"Tumepita katika Shule zetu za Msingi na Sekondari tumefanya ufuatiliaji na hata Mkurugenzi wetu amepita pia, ameona mazingira ya uandaaji wa chakula kwa baadhi ya Shule siyo mazuri, hakuna sehemu maalum kama majiko kwa ajili ya kupikia chakula".
Kamati imependekeza kuwe na mpango wa ujenzi wa majiko kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kupikia chakula Mashuleni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.