Ziara ya Naibu Waziri anayeshughulikia Afya ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, alipozuru Manispaa ya Kinondoni, Kata ya Mabwepande kukagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mabwepande kwa lengo la kujiridhisha na hatua za utekelezaji wake zilizofikiwa ikiwa ni pamoja na ubora wa mradi unaoenda sambamba na thamani ya fedha.
Akiwa katika Hospitali hiyo alipata fursa ya kuzungumza na wakina mama pamoja na kukagua word za wagonjwa, chumba Cha upasuaji pamoja na jengo la Mochuari
Ziara hiyo imehudhuriwa pia na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Pamoja na Ofisi ya Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.